Azama Baharini na kupoteza Maisha

Wafanyakazi na Viongozi wa mahoteli wametakiwa kuwa makini na waangalifu kwa wateja wao wanaofika katika maeneo ya hotelini ili kuepusha vifo visivyo vya lazima.

Wito huo ameutoa Kamanda wa Polisi Mkoa Wa Kusini Unguja Kamishna Msaidizi Muandamizi wa Polisi Suleiman Hassan Suleiman kupitia tukio la kuzama Baharini Raia wa Israel aliefika katika hotel Ya Karafuu iliyoko Michamvi Wilaya ya Kati Mkoa Wa Kusini Unguja.

Kamanda Suleiman ameeleza tukio hilo lililotokea januari 5 majira ya saa 10:15 jioni huko hotel ya Karafuu iliyoko Michamvi .

Amemtaja Marehemu huyo kuwa Saliman Karny(76) Muisrael wa Karafuu hotel Michamvi alizama baharini na hatimae alifariki dunia wakati akiongelea.

Marehemu huyo amehifadhiwa katika hospital Ya Mnazi Mmoja  kwa ajili Ya uchuguzi na baada Ya kufanikisha uchuguzi wao itafanyiwa taratibu kwa ajili Ya kusafirishwa na kukabidhiwa jamaa zake kwa mazishi.

Kamanda Suleiman ametoa wito kwa wahusika wa mahotel kuangalia wateja wao wanapofika katika fukwe za bahari ilikutambua katika kuongela kuna juliikana Au laa kwani kuongelea ni moja Ya starehe hivyo basi kunahitaji umakin wa hali ilikuepusha vifo.

Rauhiya Mussa Shaaban