Baada ya kupokea kichapo cha goli 3-0 KVZ waitupia lawama ZFA

Kocha wa KVZ Sheha Khamisi ameeleza sababu ya kupoteza mchezo wake wa kwanza jana dhidi ya Mafunzo baada ya KVZ kupokea kichapo cha magoli matatu kwa bila.

Kocha huyo ameshusha lawama sana kwa kamati ya mashindano ya ZFA baada ya kufanyika mabadiliko ya ratiba ya mchezo huo uliokuwa uchezwe majira ya saa kumi za jioni na kuchezwa majira ya saa nane kinyume na makubaliano ya kikao cha matayarisho ya mechi.

Aidha Sheha amesema KVZ watandelea kujipanga na michezo inayofuata licha ya ligi kuu ya Zanzibar kuonekana ngumu msimu huu ila mandalizi yao ni kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Zanzibar msimu huu.

Kuhusu kutoka sare kwenye Uwanja wa Kiwengwa dhidi ya Polisi Sheha amedai uwanja wa Shamba hauna nyasi nzuri ukilinganisha na uwanja wa Amani kutokana na uwanja ule kuwa hauna viwango hivyo michezo ya uwanja wa kiwengwa inakua migumu kulinganisha na uwanja wa Amani.

Kvz wako kileleni mwa ligi kuu ya Zanzibar kwa sasa wakiwa na alama 13 ,Michezo mengine ya ligi kuu ya Zanzibar imekutanisha baina ya Jang’ombe Boys wamefanikiwa kumfunga JKU goli moja kwa bila majira ya saa kumi uwanja wa Amani.

Kwa upande wa Kisiwani Pemba kwenye uwanja wa Finya Jamuhuri wamepokea kichapo cha goli 3 kwa moja dhidi ya Chipikizi, na uwanja wa Gombani Selem View wametoka sare dhidi ya Opec.

 ligi kuu ya zanzibar itandelea leo kwa kuchezwa michezo minne Uwanja wa Amani .

Malindi dhidi ya KMKM majira ya saa kumi za jioni Kiwengwa, Zimamoto dhidi ya Mlandege Amani majira ya saa kumi za jioni, Polisi dhidi ya Chuoni Amani majira ya saa kumi za jioni.

kwenye uwanja wa Gombani Mbuyuni dhidi ya Hardrock na uwanja wa Finya Mbuyuni dhidi ya Kizimbani.