Polisi Mkoani Morogoro inamshikilia mwanaume mmoja, anayejulikana kwa jina la Said Kasti (35), kwa kosa la kumbaka na kumlawiti mwanaye wa miaka 2, katika kijiji cha Kimangakene kata ya Kiloka Wilayani Morogoro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Wilbroad Mutafungwa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lilitokea siku ya Julai 8 majira ya saa 7 Usiku, ambapo mwanaume huyo alipokuwa amelala na binti yake chumbani, na ndipo alipombaka na kisha kumlawiti na kusema kiini cha tukio hilo ni imani za kishirikina.

Mwanaume huyo alifanya tukio hilo kwa imani kwamba akifanya ivo atapata utajiri, kwahiyo mwanaume huyo sisi tunamshikilia kwa ajili ya uchunguzi, na mtoto huyo kwa vile alikuwa ameumia sehemu mbalimbali za mwili wake, alipelekwa kwenye hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.

Aidha SACP Mutafungwa akatoa rai kwa wanaume. ”Jeshi la Polisi tunatoa wito kwa wanaume au watu wengine wenye mawazo potofu kama hayo, kwamba utapata utajiri kupita vitendo vya aina hiyo, me naamini ukifanya kazi ndio utaweza kutoka kimaisha na  kupata pesa na mali”

Akina mama pia wametakiwa kuwaangalia watoto, ili kuhakikisha wako katika usimamizi na malezi mazuri ya wazazi, na kuwaepusha na vitendo vya aina hiyo.