Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Bilal Hamis (61) mkazi wa mtaa wa Ushirika wilaya ya Nzega mkoani Tabora amenusurika kufa baada ya kukatwa sehemu zake za siri na mpenzi wake Veronica Ngayawula baada ya kunyimwa pesa kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Pasaka.


Inaelezwa kuwa chanzo cha tukio ni Veronica kuomba hela ya sikukuu lakini Bilal hakuwa na pesa wakati huo na inadaiwa kuwa kabla ya tukio hilo wawili hao walikuwa wanakunywa pombe.
Bilal anaendelea kupata matibabu katika hospitali ya wilaya ya Nzega.