Meneja wa Diamond Platnumz aliyepewa jukumu la kusimamia matibabu ya Hawa Said maarufu kama Hawa wa Diamond nchini India, Babu Tale ametoa taarifa ya hali ya Hawa inavyoendelea kwasasa.

Babu Tale kupitia ukurasa wake wa Insta ameandika ujumbe mrefu akielezea hali ilivyo kwa Hawa.

View this post on Instagram

Asante Mungu, asanteni watanzania kwa dua zenu. Hawa sasa yupo salama kabisa… Ameshatoa nyuzi na yupo tayari kurudi nyumbani. Haikua kazi rahisi kupitia alipo pitia, pia tunaomba muendelee kutuombea dua ili tuwe na nguvu ya kuendelea kusaidia wenzetu. Haikua rahisi kumuacha mgonjwa siku ya kwanza anatoka theatre, ila ilibidi nirudi kusimamia majukumu mengine… nikikumbuka alivyonililia mama yake mpaka nikatamani nisirudi TZ, ila majukumu mengine yalifanya nirudi. Amka uende kusali, Mungu yupo na dua pia zipo!!! maana kila nikikumbuka lile tumbo la Hawa, na Leo halipo tena… maana yake Mungu alikua anataka kuonyesha nguvu zake!! Nakumbuka aliniambia lile tumbo amekaa nalo mwaka mmoja na nusu, ila kwa nguvu ya Mungu limeondoka ndani ya mwezi mmoja, SubhanaAllah!! anasema anajiona mwembamba na mwili hajauzoea… Ijumaa Kareem

A post shared by Hamisi Taletale (@babutale) on

Kwa mujibu wa Madaktari nchini India walisema Hawa alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo na kupelekea mgonjwa kujaa maji mwilini.