Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limeagiza Misikiti yote iliyofungwa ifunguliwe mara moja ili Waislamu waswali swala ya Eid-El-Fitri kwenye nyumba hizo za ibada

Pia, BAKWATA imewataka Maimamu wote kwenye Mkoa wa Dar kufanye dua ya shukrani Ijumaa ya Mei 22 kama alivyoagiza Rais Magufuli kutokana na kile kinachoelezwa kuwa nchi imepata unafuu katika maambukizi ya CoronaVirus

Hata hivyo kila muumini anatakiwa kuchukulia Udhu nyumbani na ikiwezekana kila mtu aende Msikitini na mswala wake. Watu watatakiwa kunawa mikono kabla ya kuingia kwenye Misikiti ili kuendeleza kutokuenea kwa maambukizi