Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania CDF Venas Mabeyo Kushoto akimpokea Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Nyumbani Kwake  Kawe Jijini Dar es salaam alipofika kumpa pole baada ya kufiwa na Mtoto wake Nelson Venas Mabeyo.
 Balozi Seif Ali Iddi kushoto akiwafariji na kuwapa pole Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania CDF Venas Mabeyo na Mkewe Mama Tina Babeyo Nyumbani kwao Kawe Jijini Dar es salaam.
 Balozi Seif  Kulia akimuaga Mkuu wa Majesh CDF Mabeyo na kumtaka yeye na Familia yake kuwa na subira katika kipindi cha msiba wa Mtoto wao Kipenzi Nelson Venas Mabeyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkagua na kumfariji Muasisi wa Chama cha TANU  na Balozi wa Zamani  wa Tanzania Mzee Job Lusinde aliyelazwa Hospitali ya Rufaa Muhimbili akipatiwa huduma za Afya kutokana na matatizo ya Miguu.
 Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akimtakia Afya njema Muasisi wa Chama cha TANU  na Balozi wa Zamani  wa Tanzania Mzee Job Lusinde aliyelazwa Hospitali ya Rufaa Muhimbili akipatiwa matibabu.