Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema kutakuwa na utaratibu mpya wa kuondoa mizigo bandarini ambapo wananchi wa kawaida wataruhusiwa kutoa mizigo yao bila ya kuwa na ulazima wa kutumia Wakala wa Forodha (Clearing and Forwarding Agents).

Dkt. Mpango alisema utaratibu huu hautahusisha mizigo inayopitishwa hapa nchini kwenda nje ya nchi (Transit Cargo).

Aidha, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) itaandaa utaratibu wenye kueleweka kwa urahisi ili kuwawezesha Wananchi kugomboa mizigo yao kwa gharama nafuu zaidi na bila kuchelewa

Waziri Mpango alisema ili kuondoa malalamiko ya wafanyabiashara dhidi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Serikali imeamua kuanzisha kitengo huru cha kupokea malalamiko na taarifa za kodi (Office of Tax Ombudsman) ambacho kitaratibiwa na Wizara yake.

Aidha, alisema kitengo hicho kitahusisha kupokea na kupitia malalamiko ya taarifa za kodi zitakazotolewa na walipakodi au watu wenye nia njema