Baraza la Manispaa Mjini Unguja, Limewataka wananchi wa Wilaya ya Mjini kuzingatia usafi katika maeneo yanayo wazunguka ili kujikinga na maradhi ya mripuko.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Mjini Nd. Said Juma Ahmada wakati alipokua katika  zoezi la usafishaji wa majaa ya Manispaa ya Mjini. Mkurugenzi huyo ameongezea kwa kusema kuwa wanafanya operesheni ya usafi ya kuondosha taka katika majaa yote ya manispaa mjini ili kuweka mazingira ya mji safi.

Pia Mkurugenzi huyo alisema changamoto kubwa inayotokea katika majaa hayo ni kuwa taka hazitupwi kwenye sehemu husika ambayo ni makontena ya kuhifadhia taka pia baadhi ya wazee wanawapa taka watoto ambayo si vizuri kwa watoto kuwapa kazi hiyo ya kwenda kutupa taka kwani wakifika huwa wanatupa taka hizo chini ya Makontena ya kuhifadhia taka.