Baraza la Manispaa Wilaya ya Mjini limeanzisha sheria za papo kwa papo ili kudhibiti utupaji taka kiholela.

Hayo yamebainishwa na afisa habari wa baraza hilo Hassan Yahya wakati akizungumza na zanzibar24 huko ofisini kwake Malindi Mjini Unguja.

Amesema sheria hiyo ya papo kwa papo itawahusu wale wote wanaotupa taka sehemu zisizoruhusiwa pamoja na sehemu za bustani.

Aidha Hassan amesema katika utekelezaji wa sheria hiyo watatoa elimu katika ngazi ya shehia ili kila mwananchi kuitambua kwa lengo la kuepusha Matatizo baadae.

Baadhi ya wananchi wamesema sheria hiyo iliyoanzishwa ni nzuri na itasaidia kuweka mji katika hali ya safi.

Wamesema iwapo sheria hiyo itafanyakazi ipasavyo itasaidia kujiepusha maradhi ya Mripuko ikiwemo kipindupindu.

Rauhiya Mussa Shaaban