Wagombea waliojitokeza kugombea nafasi ya Uraisi wametakiwa kuacha kuanzisha makundi endapo miongoni mwao watatokea kushindwa na badala yake waungane kuwa kitu kimoja ili kukipatia ushindi chama .

Rai hiyo imetolewa na baraza la wazee Wa chama cha mapinduzi wakati wakizungumza na vyombo vya habar katika ofisi ya wazee kisiwandui .

Mwenyekiti Wa jumuiya hiyo Bi Khadija Mohammed amesema ni vyema wagombea wote kuwa kitu kimoja endapo wengine watatokea kushindwa  na si vyema kuanzisha makundi kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na maadili ya chama hivo ni vyema kushirikiana  ili kukiletea ushindi chama .

Kwa upande wake Katibu Wa baraza hilo  Wazir Ali Amewataka wanachama kuwa na ushirikiano Wa hali ya juu ili kuhakikisha mgombea atakayeshinda wanamapatia ushirikiano ili aweze kuleta maebdeleo ya wazanzibar .

Aidha baraza hilo limewapongeza wagombea wote waliojitokeza kwani wameonesha uzalendo na kiu ya kukipatia ushindi chama .