Wakati waislamu wote nchini wakiwa wanaelekea kusherehekea skuku ya Eid el haji Baraza la manispaa mjini limewataka wananchi kusherehekea sikuku huku wakiwa wamechukua tahadhari ya kuwalinda watoto wanao kwenda nao katika viwanja vya sikuku.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Mjini Unguja Said Juma Ahmada wakati alipo fika katika maeneo ya viwanja vya skuku Mnazi Mmoja.

Ahmada ameongezea kwakusema kua wafanya biashra wanatakiwa
kuzingatia kanuni na sheria zilizo wekwa katika viwanja hivyo.

Aidha Mkurugenzi huyo ameongezea kwakusema kua wafanya biashara
wamefika kwawingi kuomba kufanya biashara na zaid ya wafanya biashara miambili 200 wana tarajiwa kufika kufanya biashara katika viwanja vya mnazimoja.

Kwaupande wao wafanya biashara Ibrahim Ali Hassan na Suleiman Ali Mussa Wamelishukuru baraza la manispaa mjini kwa kuwaboreshea maeneo ya kufanyia biashara zao na kuwataka wafanya biashara wenzao kuzingatia usafi katika maeneo yao walio patiwa.