Wananchi wa Benin wanashiriki uchaguzi wa wabunge wapya bila wagombea wa upinzani, Tume ya uchaguzi mwezi uliyopita uliviidhinisha vyama viwili vya kisiasa vinavyodaiwa kumuunga mkono Rais Patrice Talon – kushiriki uchaguzi huo baada ya kufukia masharti yaliyowekwa.

Sheria mpya ya uchaguzi ilizitaka vyama kulipa ada ya dola 424,000 ili viruhusiwe kushiriki uchaguzi huo.

Huduma ya intaneti zimedhibitiwa huku mitandao ya kijamii na huduma ya kutuma na kupokea ujumbe mfupi zikifungwa katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Wapiga kura milioni tano wamesajiliwa kushiriki zoezi hilo katika taifa linalojivunia kuwa na utawal thabiti wa kidemokrasia.

Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wamekosoa hatua ya kuzuiliwa kwa maandamano ya amani na kukamatwa kwa wanaharakati wa upinzani wanaolalamikia hatua ya upinzani kufungiwa uchaguzi huo.