Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemuhukumu kunyongwa hadi kufa mwanamke Esther Lyimo (47) baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mjukuu wake Naomi John (7) kwa kipigo

Hukumu hiyo imesomwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi tisa wa upande wa mashtaka na utetezi

Hakimu amesema, upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa kifo cha Naomi kimetokana na kipigo na majeraha kutoka kwa bibi yake hivyo ametiwa hatiani kwa kosa la kumuua kwa kukusudia Naomi John

Mshtakiwa alimpiga marehemu, kumng’ata mwilini na kisha kumwagia maji ya moto ya chai ambapo inadaiwa ilikuwa tabia yake kumfanyia ukatili marehemu Naomi.