Wito wa usaili ofisi ya baraza la wawakilishi, Zanzibar

Tume ya Utumishi Baraza la Wawakilishi Zanzibar inawaaarifu vijana ambao wameomba nafasi za kazi katika Ofisi ya Baraza la Wawakilishi kwa nafasi za Unguja kufika kwenye usaili katika Ofisi za Baraza Chukwani siku ya Jumamosi na Jumapili ya tarehe 13 na 14 Oktoba, 2018 saa 2:00 za asubuhi.

Orodha za wasailiwa zinapatikana katika Ofisi za Baraza la Wawakilishi Chukwani kuanzia siku ya Alhamis ya tarehe 11 Oktoba,2018.

Kwa wale watakaobahatika kuona majina yao wanatakiwa wachukue vyeti vyao halisi vya kumalizia masomo, Cheti cha kuzaliwa pamoja na kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi siku ya Usaili.

 

Bonyeza hapa kupa listi nzima ya majina ya walio itwa katika usaili baraza la wawakilishi zanzibar

BLW-Wito-wa-usaili