Mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi amefuta kesi aliyoifungua Mahakama ya Juu nchini humo akipinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2021.

Bobi Wine alifungua madai ya kupinga ushindi katika uchaguzi wa rais Yoweri Museveni akidai uchaguzi uliofanyika jana Alhamisi Januari 14, 2021 ulitawaliwa na wizi wa kura ambao haujawahi kufanyika katika historia ya chaguzi za nchi hiyo.