Mkongwe wa tasnia ya vichekesho nchini Mzee King Majuto amefariki jioni ya leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokua amelazwa.

Taarifa kutoka kwa watu wake wa karibu zimethibitisha kutokea kwa kifo cha gwiji huyo wa sanaa ambaye amejizolea umaarufu kila pembe ya Nchi yetu.

Mzee Majuto ambaye alijizolea umaarufu mkubwa kwenye filamu alianza kuugua mwaka jana na mwaka huu serikali kwa kushirikana na wananchi walichanga pesa na kumpelekeka kwenye matibabu nchini India.

Muigizaji huyo alizaliwa mwaka 1948 jijini Tanga na kusoma shule Msambwini, Tanga, alianza kuigiza 1958 akiwa na umri wa miaka 9.

Taarifa zaidi ya wapi ulipo msiba na taratibu zote za mazishi zitakujia baada ya kuwasiliana na familia ya marehemu.