Ama kwa hakika kila nafsi itaonja mauti ila siku na saa ni siri yake muumba, hakika huu ni msiba wa taifa Tanzinia inalia kwa kumpoteza kiongozi wake mahiri, jasiri mwenye uchungu na mapenzi na nchi yake.

Siku ya tarehe 24 julai 2020 ni siku isiyosahaulika kwa watanzania kwa kumpoteza aliyekuwa Rais mstaafu Benjamin William Mkapa.

Benjamin William Mkapa  Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1995-2005) kupitia Chama Cha Mapinduzi, CCM alizaliwa Novemba 12, 1938 huko Ndanda Masasi Mkoani Mtwara.

Mnamo Mwaka 1995, Marehemu Benjamin Mkapa aliteuliwa na Chama Cha Mapinduzi kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Benjamini William Mkapa aliwahi kuwa Mbunge na Waziri wa Mambo ya Nje na akahudumu kutoka mwaka 1977 – 1980. Baadaye Aliteuliwa kuwa Waziri wa Habari na Utamaduni kati ya mwaka 1980 – 1982.

Benjamin William Mkapa amefariki dunia na Julai 24, 2020 wakati akiwa anapatiwa matibabu Hospitali Jijini Dar es salaam na kuzikwa Julai 29 huko kijijini kwao Lupaso Masasi Mkoani Mtwara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Rais mstaafu Jakaya Kikwete wakiweka shada la maua kwenye kaburi la Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa katika Mazishi yaliyofanyika katika Kijiji cha Lupaso Masasi Mkoani Mtwara.

Watanzania watamkumbuka kwa mengi mazuri aliyoacha na ataendelea kuishi nyoyoni mwao hakika hili ni pigo kwabwa kwa Tanzania .

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi Amina.