Nchi ya Burkina Faso imeanza maombolezo ya siku 3 ya kitaifa, baada ya kuuawa kwa watu 38 katika shambulio la kushtukiza lililotekelezwa na Wanajihadi wa Kiislamu Kaskazini mwa nchi hiyo.

Rais wa nchi hiyo, Roch Marc Christian Kabore amesema kilichotokea ni pigo kwa Taifa na kuwataka wananchi kuungana kuhakikisha wanayashinda makundi ya kijihadi.

Amelitaja shambulio hilo dhidi ya msafara wa magari ya wafanyakazi wa Kampuni ya Madini ya Semafo, kama uhalifu wa hali ya juu unaolenga kuzua hofu kwa wananchi na kuhatarisha Demokrasia.