Callisah aipatia ushindi Tanzania, aibuka kidedea Mister Africa International 2018

Mwanamitindo wa kiume Tanzania, Callisah ameibuka mshindi wa Mister Africa International 2018 katika mashindano yaliyofanyika nchini Nigeria.

Shindabo hilo lilifanyika mwishoni mwa Wiki iliyopita nchini Lagos, Nigeria na kushirikisha washiriki kutoka nchi mbali mbali za Afrika Kama vile Lesotho, Nigeria, Ghana, Cameroon na nyinginezo.

Nchi zilizomfuatia na nafasi walizoshika ni :

1.Tanzania
2.Sierra Leone
3.Nigeria
4.Ghana
5.Cameroon

Katika hatua nyingine, Mtanzania Jihan Dimack aibuka mshindi wa 3 katika Miss University Africa 2018.

Ukiacha Hilo, Jihani amewahi kuwa Miss Ilala, Miss Tanzania no.3, Miss Universe Tanzania na mwanamitindo bora Swahili Fashion Week.