Wizara ya Mambo ya Nje ya Canada imetangaza kuwaondoa raia wake 188 waliokuwa katika mji wa Hubey nchini China

Wananchi hao wamesafirishwa kutoka nchini humo kufuatia janga la coronavirus vilivyoikumba China tangu mwishoni mwa mwaka 2019

Watu zaidi ya 1100 wameshafariki kutokana na coronavirus vinavyosababisha maradhi aina ya Covid-19

Nchini Canada, ni watu 7 ambao wamepimwa na kukutwa na #coronavirus