Msanii wa muziki hip hop nchini Marekani,  Cardi B ameshinda tuzo ya Grammy kupitia album yake inayoitwa Invasion of Privacy, katika kipengele cha albamu bora (The Best Rap Album).

Tunzo hizo zimefanyika usiku wa kuamkia leo, Card B anakua ni mwanamke wa kwanza kushinda tuzo hiyo kama solo artist.

Pia wimbo wa Childish Gambino unaokwenda kwa jina la This is America ukiweka rekodi ya kuwa wimbo wa kwanza wa rap kushinda Grammy kwenye kipengele cha wimbo wa mwaka (Song of The Year).


Licha ya ushindi huo, Vazi la Cardi B alilovaa kwenye ugawaji wa tuzo hizo linazungumziwa zaidi hasa mitandaoni kutokana na muonekano wake.