Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Moudline Cyrus Castico amewataka wazazi na walezi kuendelea kuwalea Watoto wao katika malezi bora na kuwapatia matunzo yanayostahiki kwa Watoto wao.

Kauli hiyo ameitoa katika mafunzo ya uzinduzi wa vuguvugu ya malezi bora na mafunzo kwa familia katika kuelekea katika kuadhimisha siku ya Familia Dunia inayotarajiwa siku 15 Mei ya kila Mwaka Huko Ofisini Kwake Mwanakwerekwe Wilaya Magharibi B.

Amesema suala  la malezi linalenga kuhamasisha utayari katika sekta zote za jamii ya wazanzibar kushiriki na kuunga mkono kina mama na kina baba pamoja na walezi kuimarisha familia zao na kuendeleza familia bora kuwapenda,kuelea na kupata ustawi wao watoto.

Hata hivyo Afisa wa Idara ya maendeleo ya Wanawake na Watoto Mohammed Jabir amesema kuwa mikakati ya kuhamasisha na kuwajengea uelewa kwa jamii kupitia uwajibikaji katika malezi bora na makunzi  bora na ulinzi kwa Watoto.

Sambamba na hayo waandishi wa habari wamepata kuuliza masuala mbali mbali na kupatiwa ufumbuzi ikiwemo masula ya udhalilishaji wa kijinsia pamoja na mimba za utotoni.

Maadhimisho ya Siku ya Familia Dunia kuadhimishwa kila ifikapo Mei kumi na tano kila Mwaka na kutarajiwa kufanyika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakili KiKwajuni na Mgeni Rasmi Wazir wa Elimu na Mafunzo Ya Mali Riziki Pembe Juma.