Chama cha Mapinduzi (CCM) kimefanikiwa kuchukua jimbo la Buyungu kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge kwa ushindi mnono dhidi ya vyama vya upinzani.

CCM kupitia kwa mgombea wake wa Ubunge, Chiza C. Kajoro amepata ushindi kwa kura 24,578 huku Elia F. Michael wa CHADEMA akipata kura 16,910.

Kwa upande wake Mgombea wa CHADEMA, Elia Michael amesema kuwa amepokea matokeo hayo na amekubaliana nayo huku akiahidi kujipanga upya kwenye uchaguzi ujao.

Nimejifunza kutokana na uchaguzi huu, na umenijenga kwa kiwango kikubwa. Ninashukuru kwamba nimepewa fursa ya kushiriki miaka mingine tutaonana mimi umri unaruhusu. Kwa vile mimi bado ni kijana yote haya nachukua kama ni changamoto sipo tayari kupambana kwa sababu ya madaraka.amesema Elias jana usiku kwenye mahojiano yake na NEC TV.

Jimbo la Buyungu lilikuwa wazi tangu mwezi Mei mwaka huu baada ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Kasuku Bilago (CHADEMA) kufariki dunia.