Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Rodrick Mpogolo, amewapokea wanachama wapya wa chama hicho kupitia kampeni ya Dar ya Kijani inayoratibiwa na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam.

Kampeni hiyo ya Dar ya Kijani ina lengo la kurudisha mitaa, kata na majimbo yote katika himaya ya chama, inawataka vijana na wanachama wote kuimarisha ushirikiano na kupata ushindi wa pamoja wenye heshima kwa chama hicho tawala.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kwa Wilaya ya Kinondoni, Mpogolo, amewataka vijana kuwa makini na waadilifu kwani wao ndio wataokaojenga hehima ya chama na Taifa kwa ujumla.

“Vijana ndio tunao wategemea katika uchaguzi ujao tunahitaji vijana makini na waadilifu ambao watakitumikia chama chetu cha Mapinduzi na Serikali yetu. jiepushieni mbali na tabia ambazo zitawaondelea maadili yenu. Ili mkawe viongozi makini kwani taifa letu linaitaji viongozi makini na wachapakazi.

Amesema tangu kampeni hiyo ilipozinduliwa Machi 17, mwaka huu jijini Dar es Salaam imefanikiwa kuvuna zaidi ya wanachama 500  ambao wamejiunga na chama hicho