Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kitaendelea na msimamo wake wa kutomuunga mkono Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba ikiwa ni siku chache tangu upande wa Maalim Seif kutangaza nia ya kumuunga mkono mgombea wa jimbo la Liwale, Mohamed Mtesa ambaye pia anaungwa mkono na Profesa Lipumba.

Akizungumza na Eatv Mkurugenzi wa Sera na mahusiano ya Nje wa  CHADEMA, John Mrema kuhusiana na kauli yao kama moja ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kufuatia muungano baina ya pande hizo mbili zenye mgogoro wa kiuongozi.

Katiba ya CUF inasema  anayepitisha mgombea nafasi ya ubunge ni ngazi ya wilaya, ndio maana sisi tunamuunga mkono Katibu Mkuu Maalim Seif, hatuwezi kumuunga mkono Lipumba aliyejiuzulu, na hata kama akiituomba radhi kama UKAWA hatutaki kuombwa radhi na yeye muhimu Lipumba atambue anaongoza taasisi, kwa hiyo afuate taratibu tu.”, amesema Mrema

Hivi karibuni, Naibu Mkurugenzi wa Habari CUF anayemuunga mkono Maalim Seif, Mbarara Maharagande alisema kiongozi wao atafunga kampeni jimbo la Liwale kuelekea uchaguzi huo utakaofanyika mwezi huu baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Zuberi Mohamed kuhamia CCM.

Sisi upande wetu hatuna tatizo, kwa sababu yule ni mwenyekiti wetu wa halmashauri na viongozi wetu wameshaelekea huko kumuunga mkono, na Maalim Seif wiki hii anatarajia kwenda kufunga kampeni, Sisi ndio tulimwambia akachukue fomu na apitishe kwa upande wa Lipumba kwa sababu ndie anayetambuliwa na dola.”, amesema Maharagande.