Chama cha Alliance for Democratic Change ADC kimesema kinatarajiwa kufanyaa mkutano  mkuu Zanzibar ambapo katika mkutano huo utawapa fursa wanachama kufanya uchaguzi wa kuchagua viongozi wapya katika chama hicho.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katika ukumbi wa Idara ya habari maelezo Mjini zanzibar Katibu Mkuu wa Chama cha ADC Doyo Hassan Doyo amesema uchaguzi huo utawawezesha wananchi kuchagua viongozi kulingana na sheria na taratibu za katiba ya chama hicho.

Amesema Mfumo wa chama ni kufanya uchaguzi wa viongozi ili kuwapa fursa wanachama wengine kuweza kuwania baadhi ya nafasi zitakazogombaniwa kwa maslah ya chama.

Amesema mbali na Uchaguzi pia Mkutano huo unatarajia kuzindua mpango mkakati wa cha hicho utakaotekelezwa na wanachama wa Tanzania.

Amesema mpango huo baada ya kuzinduliwa utawawezesha wanachama kuwa na uzalendo WA chama chao kwa lengo la kufikia malengo ya kuchangia maelendele na kushinda katika uchaguzi mkuu ifikapo 2020.

Aidha katibu mkuu huu amesema pia katika mkutano huo watafanya marekebisho baadhi ya Vipengele vya katiba ambavyo vinamapungufu katika katiba ya Chama cha ADC.

Amesema miongoni mwa kipengele kitakachofanyiwa marekebisho ni pamoja na kipengele cha Vikundi vya Ulinzi na Usala ili viweze kuendana na mahitaji.

Hata hivyo Katibu Doyo ameiomba serikali kuwaruhusu kufanya mikutano badala yake wadhibiti Vyama vinavyofanya mikutano kinyume na taratibu za nchi ikiwemo kufanya maandamano .   “Tunaiomba serikali ituruhusu kufanya mikutano kwa sababu sisi hatuna wabunge wala diwani hivyo kupitia mikutano yetu ndo tunajadili matatizo na namna ya kuimarisha maendeleo yetu kwa wanachama”. Alisema KATIBU Doyo

Kwa upande wake Naibu katibu Mkuu wa ADC Queen Cuthbert Sendiga ametumia fursa hiyo kuwataka wanawake kuwa mstari wa mbele katika kuwania nafasi za uongo ili waweze kujitatulia matatizo yanayowakabili.

Amesema Chama hicho kinampa fursa Mwanamke kuwania nafasi za uongozi hivyo si vyema kuwa nyumaa kujitokeza kuwania nafasi hizo.

Amesema katika kuhakikisha wanawake wanakuwa na ushiriki mzuri katika kuwania nafasi hizo chama kitaendelea na utaratibu wa kutoa elimu kwa vijana na wanawake ili kuwajengea uwezo wa kuwa viongozi bora katika uchaguzi mkuu ifikapo 2020.

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika April14 mwaka huu katika ukumbi wa Madinatul bahri Bweni Nnje kidogo ya mji wa Zanzibar na kushirikisha viongozi na wanachama wote wa ADC ambapo lengo kuu ni kuzindua mkakati wa Chama hicho.

Na;fat-hiya Shehe Zanzibar24