Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC) Abdallah Manzi Yussuf amesema Chama cha Mapinduzi hakitomfumbia macho Kiongozi yoyote  atakaeshindwa kutekeleza Ilani ya Chama hicho na jina lake halitorudi wakati atakapoomba ridhaa kwa mara nyegine.

Amesema haiwezekani kuona Viongozi wakuu akiwemo Raisi wa Jamuhuri ya Muungano Dkt John Pombe Magufuli na yule Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein tayari wamekekeleza Ilani kwa zaidi ya asilimia 95 lakini baadhi ya Wabunge,Wawakilishi na Madiwani wanashindwa kutekeleza ahadi walizoweka na kubaki kama Mzigo.

Ameyasema hayo huko katika ofisi ya ccm Nyerere wakati alipokuwa akikabidhi kadi kwa Wanachama wapya wa Jimbo la Amani ikiwa ni shamrashamra za kutimiza miaka 42 ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Amefahamisha kuwa Viongozi hao wameomba nafasi za Uongozi bila kulazimishwa na mtu lakini baaadae wanashindwa kuwatumikia Wananchi jambo ambalo linasababisha baadhi ya Wanachama kukosa Imani na Viongozi hao.

Mbali na hayo amesema zipo taarifa kuwa kuna baadhi ya Wanaccm wameanza kupita mitaani na kupiga kampeni kuomba ridhaa ya kuongoza nafasi za Ubunge,Uwakilishi na Udiwani jambo ambalo halivumiliki hata kidogo kwani linaweza kuleta migogoro kati yao na Viongozi waliopo Madarakani.

Amesema hata siku moja Ccm haitokubali kuona Viongozi hao wanaomba ridhaa ya kuwatumikia Wananchi ili wawatumikie kwa kuwatatulia matatizo yanayowakabili na kuwaletea maendeleo katika maeneo yao lakini wanashindwa kutekeleza ahadi wazilizoziweka kwa Wananchi hao.

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa CCM Jimbo la Amani Bi Tuwalelee Mbwana Hamad amesema kukabidhi kadi Wanachma wapya ni miongoni mwa maandalizi ya mikakati ya kukipatia ushindi Chama Cha Mapinduzi ifikapo mwaka 2020.

Takdir Ali.