Uchunguzi uliofanywa kwa chanjo mbili tofauti za ugonjwa wa Ebola umebaini kuwa chanjo hizo zinaweza kumkinga mtu kutokana na virusi vya ugonjwa wa Ebola kwa takriban mwaka mmoja.

Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la New England Journal of Medicine, ulifanyika huko nchini Liberia na kuwashirikisha wagonjwa 1,500

Watu wote waliopewa chanjo hiyo walifanikiwa kupata kinga yenye nguvu kwa karibu mwaka mmoja.

Majaribio hayo yanaonesha kuwa chanjo hizo zote zinaweza kutumiwa kuokoa maisha wakati wa majanga ya ugonjwa wa Ebola siku za usoni.

Ugonjwa wa Ebola uliwaua zaidi ya watu 11,000 nchini Liberia, Sierra Leone na Guinea, wakati wa mripuko wa ugonjwa huo mwaka 2014-2015.