Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mkali wa michano (free style), Rashid Makwilo maarufu kama Chid Benz, amefunguka mipango yake ya kuachana na muziki na kumtumikia Mungu.

Akizungumza na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Chid benz amesema kwamba kitendo cha kukutana na Sheikh Abdulrazac ni kama moja ya njia ya kufikia malengo yake, kwani anamsaidia kumkuza kiroho.
chidi

Chid benz akiwa na Sheikh Abdulrazac

“Muziki ni kitu hatari sana, kama hivi unaona niko na sheikh maana yake kuacha maisha hayo ya muziki na stori za muziki tunahitaji watu kama hawa, ili watufundishe mambo hayo ya huku, katika maisha sisi vijana tunavyoishi tunasafiri kule na huku, mimi naweza muziki sana, yeye anaweza kurutubisha maombi yako na yake yaungane kuyasogeza kwa mwenyezi Mungu, ni yeye anisaidie mimi kwa njia gani niweze kufikisha maombi yangu kwa mwenyezi Mungu, inawezekana naomba kila siku lakini hunisikii kutokana nina uchafu labda”, amesema Chid Benz

Chuchu Hans awatolea povu mashabiki wanaokosowa movies

Ikumbukwe kwamba sheikh huyo hivi karibuni aliweka wazi mipango yake ya kumbadilisha Chid Benz ili aache muziki na kumtumikia Mungu, hususan kwenye kipindi ambacho Chid anaonekana kuanza kusimama badala ya kupitia misukosuko mingi kwenye maisha ya sanaa na ujana.

Iwapo Chid Benz atafikia hatua hiyo, ataungana na Mzee Yusuph, Suma Lee na Saigon, ambao waliamua kuacha bongo fleva na kuwa waumini wazuri wa dini huku wakimtumikia Mungu.