Staa wa muziki duniani Chris Brown afufunguliwa mashtaka mapya mahakamani na mzazi mwenzake Nia Guzman kwa kosa la kutotoa pesa za huduma ya matumizi kwa mtoto.

Nia Guzman amesema amefungua mashtaka hayo baada ya kuona Chris Brown amegoma kulipa shilingi milioni 40 alizoambiwa alipe na mahakama mwezi wa pili mwaka huu.

Nia Guzman ambaye ana mtoto mmoja na Chris Brown aitwae Royality,

“Huwa hashiriki katika kutoa msaada wa matumizi ya mtoto wake na gharama zimeongezeka, huwa anapuuza matangazo yanayotolewa na mahakama katika suluhisho ya malezi ya mtoto. Nataka kurejeshewa gharama zangu zote nilizokuwa natoa tangu mwanzo wa kesi, pia alipie thamani ya nyumba aliyokubali kulipa, jumla nataka milioni 592”

Aidha mama wa mtoto huyo amedai kuwa kwa sasa anapitia wakati mgumu wa kumlea mtoto huyo kwa sababu hana kazi na hapati msaada wowote kutoka kwa Chris Brown ambaye anaingiza kiasi cha bilioni 16 kwa mwaka.

Mbali na kesi hiyo mama huyo amesema anataka milioni 15 kwa kila mwezi kwa matumizi ya mtoto huyo, japo kuwa Chris Brown mwenyewe aliwahi kulalamika kuwa mama mtoto huyo huwa anaongeza pesa kwa aajili ya matumizi yake binafsi.