Chuchu Hans awatolea povu mashabiki wanaokosowa movies

Msanii wa bongo movies Mwanadada Chuchu Hans amefunguka na kuwatolea povu mashabiki kwa kuwaambia kuwa waekuwa wakikosoa movies kila siku bila kujua undani wa  vitu hivyo.

wikiendi hii kuna picha ilipostiwa katika page nyingi za udaku zikimuonyesha  mwanadada huyo akiwa katika moja ya sehemu ya filamu zake akifanya kazi huku akiwa katika jeneza lakini akiwa hajafumba macho , picha iliyowafanya mashabiki weng kuongea na kuponda sana thamani ya bongo movies.

“Sio kila kitu mnakuwa tu manakosoa hapa hii picha tulikuwa hata hatujaanza kushoot, nadhani muangalie na muvi na ndio mkosoe.” amesema Chuchu

katika movie hiyo ambayo ipo jikoni, inaitwa Laura na pia yupo mwanadada anaefanya vizuri Esha Buheti, lakini hakuna kitu walichokiona  ambacho wao wanakiponda sio kweli, na movie hii ni ya kitambo kidogo na hata picha zake ziliwahi kuonyeshwa katika swahili world kwa ajili ya kuitangaza movie na haina vitu mabavyo mashabiki wamevipond.