Chuimilia wa miaka minne katika bustani ya wanyamapori (Zoo) Jijini New York amethibitishwa kuwa na maambukizi ya Coronavirus ikiwa ni mara ya kwanza kwa mnyama kuumwa baada ya kupata maambukizi kutoka kwa binadamu

Bustani hiyo ya Bronx katika mji wa New York, inasema kwamba matokeo hayo ya Chui huyo anayejulikana kwa jina la Nadia yalithibitishwa na maabara ya huduma ya afya ya mifugo mjini Iowa.

”Nadia, na dada yake Azul pamoja na Chui wengine wawili na Simba watatu kutoka Afrika walianza kikohozi kikavu na wote wanatarajiwa kupona kabisa,” ilisema taarifa ya uongozi wa bustani hiyo.