Kiungo wa Klabu ya Simba Clautous Chama ‘Triple C’ ameomba radhi kwa tukio la kumkanyaga kwa makusudi mchezaji wa klabu ya Yanga Feisal Salum “FeiToto” katika mechi ya watani wa Jadi iliyochezwa juzi ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa goli 1-0.

Chama kupitia Mtandao wake wa kijamii ameandika “Nina huzuni tumepoteza lakini nataka niwahakikishie kwamba kilichotokea kati yangu na Feisal kilikuwa ni binafsi walasio kwa shinikizo la matokeo ya derby, binafsi nimeongea na Feisal na amekubali msamaha wangu”