Mwanamfalme wa Uingereza Charles (71) amegundulika kuwa na maambukizi ya COVID19.

Kwa mujibu wa taarifa, Mwanamfalme alionesha baadhi ya dalili za Virusi hivyo Jumapili. Vipimo vilichukuliwa siku inayofuata na leo vimethibitisha kuwa ana maambukizi ya CoronaVirus huku mke wake aitwaye Camilla (72) ‘Duchess of Cornwall’ amepimwa na kuthibitika kuwa hana maambukizi.

Haijafahamika ni wapi Mwanamfalme Charles amepata maambukizi hayo lakini amekuwa akikutana na watu mbalimbali katika wiki zilizopita, kama sehemu ya majukumu yake.

Taarifa iliyotolewa imesema anaendelea vizuri na yupo karantini nyumbani kwake huko Scotland huku akiendelea na kazi zake.

Alikutana na Malkia Elizabeth kwa mara ya mwisho Machi 12 na imeelezwa kuwa afya ya Malkia huyo ni nzuri.