CUF ya Lipumba yavitaka vyama vya siasa kuiunga mkono Serikali

Mratibu wa uchaguzi wa chama cha wananchi Cuf Ali Makame Issa amewataka viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa nchini kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuleta maendeleo nchini.

Ali Makame Issa ambaye mratibu wa chama cha wananchi CUF kwa upande wa Prof. Ibrahimu Haruna Lipumba visiwani Zanzibar,

Alisema Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikijitahidi kwa namna tofauti tofauti katika kuhakikisha inapiga hatua katika suala zima la maendeleo.

“Suala zima la maendeleo halina chama cha siasa kwani wote lengo letu kujenga nyumba moja”alisema Ali Makame Issa.

Aidha alisema viongozi  wa vyama vya siasa wanaojitambua huwa wapo mstari wa mbele katika kuhakikisha wanaunga mkono jitihada za serikali katika kuwaletea wananchi wake maendeleo na Si kuibeza.

“Ukiwa upo katika chama cha upinzani basi haimanishi kuwa mpingaji na kuwa mtu wa kubeza maendeleo yanayofanywa na serikali pamoja na chama tawala” alisema Ali Makame Issa mratibu wa uchaguzi chama cha wananchi CUF.

Kauli hiyo aliitoa mapema wakati akitoa salamu kwa wananchi waliojitokeza kushuhudia utoaji wa zawadi kwa wanafunzi waliopata ufaulu wa Division 1 katika mitihani ya kidato cha sita mwaka 2018.

 Na.Thabit Madai, Zanzibar.