Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam imemtangaza rasmi Mhe. Abdallah Mtolea (CUF) kuwa mbunge halali wa jimbo la Temeke – Dar es Salaam, baada ya mlalamikaji, Abbas Mtemvu (aliyekuwa mgombea wa CCM) kushindwa kuithibitishia mahakama kuwa ubunge wa Mtolea ulipatikana kwa njia zilizo kinyume na sheria na taratibu za uchaguzi.