David Beckham apigwa marufuku kwa kutumia simu akiendesha gari

Mahakama imearifiwa amepigwa picha na raia akiwa ameshikilia simu wakati akiendesha gari lake aina ya Bentley ‘taratibu’ katika foleni.

Beckham, mwenye umri 44, ametozwa faini ya £750, ameagizwa alipe £100 gharama ya kesi na malipo ya ziada ya £75 katika siku saba zijazo.
Jaji katika mahakama hiyo amemuambia hata kama kasi ya gari ilikuwa taratibu kwenye foleni ‘hakuna kisingizio’ chini ya sheria.

Mwendesha mashtaka amesema: “Badala ya kutazama mbele na kuangalia barabara alionekana akitazama mapajani mwake.

Wakili wa Beckham Gerrard Tyrrell amesema mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United ” haikumbuki siku hiyo au tukio hilo”.
Aliongeza: “Hakuna utetezi wa kilichotokea, lakini mtazammo wake ni kwamba hakumbuki.”

Tyrrell ameiambia mahakama kwamba Beckham hufurahia kuendesha gari.