Mkuu wa wilaya ya kaskazini b Rajab Ali Rajab amewataka masheha  katika wilaya hiyo kuwa makini na watu wanaojitokeza katika shehiya zao kwa visingizio vya kuwa  wameagizwa na serikali kufanya kazi maalumu  kabla ya kupata taarifa sahihi kutoka  ofisi ya wilaya

Amesema katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu kuna baadhi ya watu wamekuwa wakijitokeza katika shehiya  kwa visingizio vya kufanya utafiti wa mambo mbalimbali ikiwemo suala la ulinzi na usalama  jambo ambalo linaweza kuhatarisha amani na utulivu uliopo katika.

Hayo ameyaema akizungumza na masheha  ofisini kwake mahonda amesema kisheria sheha ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika shehiya yake hivyo ni vyema kwa kipindi hiki kuwa msatari wa mbele  kuhakikisha  wanatoa taarifa  kwa uongozi wa wilaya ili waweze kuchukuliwa hatua kabla ya kuathiri jamii

Amefahamisha kuwa suala la amani na utulivu ni suala muhimu kwa wananchi hivyo ofisi yake haitakuwa tayari kuona badhi ya watu wanarudisha nyuma juhudi hizo kwa kuingia katika wilaya na kufanya utafiti bila ya kufuata taratibu za kiserikali.

mapema afisa vijana wilaya ya kaskazini b mboja ussi kali amewataka masheha hao kuhamasisha vijana katika shehiya zao kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kujiunga na mafunzo ya amali ambayo yanatarajiwa kutolewa na wizara ya vijana wazee wanawake na watoto bila ya malipo yoyote ili kila kijana aweze kunufaika na fursa hiyo

Amefahamisha kuwa serikali kwa kushirikiana na wizara hiyo imeandaa mkakati  maalumu wa kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana hao hasa kwa wanawake   pamoja na watu wenye mahitaji maalumu jambo ambalo litasaidia kuondoa tatizo la ajira hapa nchini.

kwa upande wao masheha hao wameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa uongozi wa wilaya kwa kuhakikisha serikali inafikia malengo iliyojiwekea kwa kutoa huduma bora kwa wanachi wake

Rauhiya Mussa Shaaban