Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B Rajab Ali Rajab amewataka mafundi waliokabidhiwa ujenzi wa nyumba katika  eneo la mangapwani kuongeza kasi katika ujenzi huo ili kwenda sambamba na muda waliokubaliana

Amesema  licha ya hatua nzuri  ya ujenzi  iliyofikiwa lakini bado ipo haja kwa mafundi hao kuongeza bidii ya ujenzi  ili Serikali iweze  kuanza uekezaji  katika  eneo la Bumbwini  ambalo limetengwa kwa ajili ya uekezaji wa  gesi na mafuta

Akizungumza katika ziara ya kutembelea eneo hilo la ujenzi wa nyumba huko Mangapwani DC Rajab amesema  Serikali imeamua kujenga nyumba hizo ili kulipa fidia wakaazi wa kijiji cha dundua  ambao eneo la kijiji chao limeingia katika uekezaji wa gesi na mafuta.

Hata hivyo amewataka wananchi watakaokabidhiwa nyumba hizo kuzitunza ili ziweze kudumu kwa muda mrefu na kunufaisha kizazi cha sasa na baadae

Nae msimamizi mkuu wa mradi wa nyumba hizo kutoka mamlaka ya udhibiti wa  nishati  zura bwana Zubeir Muhammmed amesema mamlaka yake tayari imekabidhi fedha zote pamoja na vitendea  kazi ambavyo  vitatumika kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo

kwa upande wao wasimamizi wa ujenzi kutoka kikosi cha mafunzo Inspector Saleh Ali na fundi mkuu kutoka kikosi cha kmkm Haji Hussein  wamesema licha ya matatizo madogo madogo yaliyojitokeza watahakikisha wanakabidhi nyumba hizo  kwa muda waliokubaliana