Mkuu wa wilaya ya kaskazin B Rajab Ali Rajab amewataka baadhi ya wananchi katika kijiji cha bumbwini makoba wanaopinga kupigwa kwa ngoma ya pungwa kuwacha wenzao waendelee na upigaji wa ngoma hiyo kwa lengo la kudumisha mila ,silka na utamaduni waliorithi kutoka kwa wazee wao

Amesema katika nchi kila mtu ana Uhuru wa kulinda na kuendeleza utamaduni wake bila ya kuvunja sheria zilizowekwa na serikali hivyo kitendo cha baadhi ya watu kuipinga ngoma hiyo kuingilia Uhuru wa watu amabao unaruhusika kisheria

Akizungumza na wananchi katika kijiji cha bumbwini makoba katika sherhe maalumu ya ngoma hiyo mkuu huyo wa wilaya amesema wananchi wa kijiji hicho wamekuwa mstari wa mbele katika kuendeleza utamaduni wao kwa imani ya kuwa ni kinga  kwao

Amesema awali kulikuwa na mgogoro ambao umefika katika mahakama na kushinda kesi hivyo uongozi wa wilaya unaheshimu maamuz ya mahakama na kuruhusu ngoma hiyo kwa kuendeleza kupigwa kwa kuzingatia kibali kilichotolewa

Aidha amewataka wananchi kuacha tabia ya kutoa kauli za vitisho kwa wenzao ambao wanaunga mkono kupigwa kwa ngoma hiyo kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha amani na utulivu katika kijiji hicho na kuahidi kuwachukulia hatua kwa atakae kiuka agizo hilo.

Ngoma ya pungwa ni miongoni mwa ngoma ambazo zinaitangaza Zanzibar kimataifa ikifuatiwa na sherehe za mwaka kogwa makunduchi,pamoja na ngoma ya msewe.