Chama Cha Demokarasia Makini kimeipongeza Serikali kwa juhudi inzaozichukuwa za kujikinga na kupunguza kuenea kwa virusi vya Corona (COVID 19) nchini.

Akitoa Taarifa kwa vyombo vya Habari, Katibu Mkuu wa Chama hicho Ameir Hassan Ameir amesema kitendo cha Serikali kufunga Skuli, Vyuo Madrasa na kuzuia mikusanyiko ya Watu ikiwemo ligi kuu ya Mpira wa Miguu itasaidia kuondosha Maradhi hayo ambayo ni Janga la Dunia.

Amesema Demokrasia Makini inaunga Mkoano hatua hiyo na kuahidi kuisaidia Serikali kuhamasisha jamii juu ya kutoa elimu ya kuzuia Mikusanyiko na Wananchi kutumia Vitakasa Mikono.

Aidha amewaomba Viongozi wa Dini,Vyama vya Siasa,Wasanii na Watu mashuhuri kuchukuwa nafasi zao kwa kuielimisha jamii ili iweze kujikinga na Virusi vya COVID 19.

Takdir Ali