Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe amesema kuwa Lowassa  hakujua mziki uliopo upinzani dhoruba za miaka miwili tu alilegea kuliko mlenda.

Mbowe amesema kuwa Chama hicho hakiwezi kufa kwaajili ya mtu.

“Na ndio maana kiongozi yeyote aliyejiaminisha kuwa akitoka Chadema chama kitakufa hiki chama hakifi kwaajili ya mtu, hata alivyokuja Lowassa tulimhifadhi tuka nia pamoja lakini pengine hakujua mziki uliopo upinzani dhoruba za miaka miwili tu mzee alilegea kuliko mlenda,” alisema Mbowe Mkoani Singida.