Diamond aahidi kufanya makubwa Tandale kwa gharama ya zaidi Tsh. milioni 465 Ijumaa hii

Diamond Platnumz anatarajia kutoa misaada ya Mitaji ya biashara kwa akina mama, pikipiki 20 kwa vijana, kukarabati shule zote Tandale, kusambaza maji na kuwakatia bima za afya kwa kaya 250  kwaajili ya wakazi wa mtaa aliozaliwa wa Tandale ambapo anakaridiwa kutumia zaidi ya tsh milioni 465 ili kuyafanikisha hayo yote.

Muimbaji huyo amedai atatoa bima za afya kwa kaya 250, ambapo kila kaya ni tsh milioni 1501200 kwa bima ya NHIF. Kwa maaana hiyo kwa kaya 250 atatumia zaidi tsh milioni 375.

Pia atatoa mitaji ya biashara kwa akina mama ambapo inakaridiwa atatumia zaidi ya tsh milioni 20 kwa akina mama 100. Alisema atagawa tsh laki moja mpaka laki mbili kwa akina mama wa Tandale.

Amesema atatoa pikipiki 20 kwaajili ya vijana ili wajikwamue kiuchumi ambapo inakadiriwa atatumia zaidi ya tsh milioni 50.

Katika hatua nyingine muimbaji huyo ambaye ni rais wa WCB, amesema atakarabati shule za Tandale pamoja na kuweka matanki ya maji ambapo ninakadiriwa atatumia zaidi ya tsh milioni 50.

Kwa maana hiyo huwenda muimbaji huyo akatumia zaidi ya tsh milioni 465 kwaajili ya kutekeleza ahadi zake hizo. Pia alisema katika kulitekeleza hilo ijumaa hii ataambatana na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wamakampuni.

Bongo5.