Msanii wa Bongo Fleva ambaye pia ni CEO wa WCB Diamond Platnumz ameeleza kufurahishwa na taarifa zilizoanza kusambaa mapema leo Novemba 9 baada ya Meneja wake Babu Tale kuuelezea umma kuwa kwasasa Afya ya msanii Hawa Said inaendelea vizuri nchini India.

Diamond ameonesha furaha yake na kuahidi kumuwezesha kibiashara mwanadada huyo pindi akirudi nchini ambapo kupitia ukurasa wake wa Insta ameandika “Nafarijika Kuona Unatabasamu sasa……nitafurahi kusikia wazo zuri la biashara toka kwako nikuwezeshe 🙏🏻 #HawaIsSmilingNow”