Diamond Platnumz kutumbuiza Maonesho ya Wajasiriamali ya ZSSF Kariakoo Zanzibar.

 

Katikati Naibu Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na watoto Mhe. Shadya Mohammed Suleiman akipiga picha na Uongozi wa Mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar ZSSF akiwemo Mkurugenzi Muendeshaji wa ZSSF Ndug Sabra Issa Machano.

Naibu Waziri wa kazi uwezeshaji wazee wanawake na watoto Mhe. Shadya Mohammed Suleiman Ameupongeza Uongozi wa mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar ZSSF kwa kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuzitatua changamoto za wajasiriamali nchini kwa kuandaa maonesho maalumu kwaajili ya kutangaza bidhaa za wajasiriamali.

Mhe. Shadya ametoa pongezi hizo wakati akifungua  maonesho ya kwanza ya wajasiriamali yaliyoandaliwa na Mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar ZSSF yanayofanyika ndani ya kiwanja cha kufurahishia watoto Kariakoo Mjini Unguja.

Amesema Serikali inaona mchango mkubwa unaotolewa na ZSSF Katika kuimarisha maisha ya wazanzibar  na ni malengo ya muda mrefu ya Serikali kutaka kuwawezesha wajasiriamali kwa kuwatatulia changamoto ya masoko ya kuuzia bidhaa zao na kuzitangaza bidhaa hizo ndani na nje ya Zanzibar.

Amesema hatua walioichukuwa ZSSF kuandaa maonesho hayo yatakayo wakutanisha zaidi ya wajasiriamali 40 kutoka Zanzibar na Tanzania bara itasaidia kuzitangaza bidhaa zao kwa kiwango kikubwa.

Awali akizungumza katika ghafla hiyo Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSSF Ndg. Khamiss  Fil fil amesema Maonesho hayo yamejumuisha wafanyabiashara wa bidhaa tofauti kote nchini, yameanza rasmi  jana Disemba 6 na yanatarajiwa kumalizika Disemba 10 ambapo yatafungwa kwa burudani kutoka kwa Mjasiriamali na msanii maarufu Nasib Abdul maarufu Diamond Platnumz akiongozana  na timu yake ya WCB.

Ndg. Khamiss amesema kuanzia tarehe iliyofunguliwa maonesho hayo hadi siku ya mwisho Wananchi wote wanakaribishwa kuja kuangalia bidhaa tofauti zilizopo kwenye maonesho hayo katika viwanja vya kufurahishia Watoto Kariakoo bila ya kiingilio chochote.

Aidha ametoa wito kwa Wajasiriamali kutumia fursa hiyo kujiunga na mfuko wa hiari ili kujiekea hakiba kwa maslahi yao ya baadae kama wafanyakazi wengine walioajiriwa na kupata pencheni zao baada ya kustaafu.

Wahida Mbaya.