Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema azma ya Serikali atakayoiunda iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa awamu ya nane ni kusimamia maslahi ya wakulima wa zao la mwani ikiwa ni pamoja na kuboresha bei ili wakulima waweze kunufaika na zao hilo.

Akizungumza na wakulima wa wa zao hilo huko Micheweni akiwa katika kamepeni ya kuomba ridhaa ya wananchi, Dkt Hussein amesema mbali na kuongeza bei za zao hilo pia pembejeo kwa ajili ya kilimo cha zao hilo zitapatikana bure.

Aidha Dkt Hussein ameahidi kubadilisha mfumo wa utoaji wa vibali kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza nchini ili kuondoa urasimu unaokwamisha maendeleo kupitia sekta ya uwekezaji.

Nao wakulima wa zao hilo wamesema changamoto kubwa ni bei ndogo ambayo hailingani na ugumu wa kazi uzalishaji wa zao.