Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema pindi atakapopata ridhaa ya kuongoza Nchi atahakikisha kwamba wakulima watapatiwa Elimu ili kuondokana na kilicho cha zamani .

Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizumgumza na wakulima kisiwani Pemba ,juu ya mikakati ya uwawezesha wakulima hao ,ilikuondokana na kilimo cha zamani kisichowaletea tija wakulima hao.

Dk. hussein amesema atahakikisha kwa jitihada zote kuwa kiwango cha wazalishaji kinaongezeka ili kukuza uchumi nchini.

Nae mmoja wakulima ndugu Mohd salum amesema watakapopewa  elimu wataweza kunufaika na kilimo ambacho ndio uti wa mgongo wa Nchiyetu.

Kwa Upande wake Mkulima wa zao la karafuu Abdalla Miraji amesema Pindi watakapopewa elimu ya kuanzisha vitalu vya kupanda mikarafuu itawasaidia kunufaika na kilimo hicho.

PICHA NA IS-HAKA OMAR,PEMBA