Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi leo Novemba 21 amewaapisha mawaziri wote aliowateuwa katika baraza jipya la mawazairi .

Akisoma hutba yake Dk.. Hussein amesema “Kila Waziri ahakikishe anaijua Wizara yake na Taasisi zilizo chini ya Wizara husika haraka iwezekanavyo, mtapewa kitabu kutoka ofisi yangu chenye ahadi zangu wakati wa kipindi cha kampeni, mpango bila bajeti ni rasimu” Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi – Rais wa Zanzibar.

“Nimetembelea baadhi ya maeneo, nimesikitishwa na kiwango cha miradi tunayoifanya, mkandarasi ameshalipwa fedha zote, nataka maelezo ya kina juu ya mradi ule” Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi – Rais wa Zanzibar