Dk.Shein awaapisha wajumbe wapya kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein jana  amewaapisha Wajumbewapya wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar.

Wajumbe walioapishwa katika hafla hiyo iliyofanyika  Ikulu mjini Zanzibar ni Dk. Mohammed Seif Khatib pamoja na Mbaraka Mohammed Abdulwakil.

Hafla hiyo, ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo Mawaziri, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Washauri wa Rais, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mzee Ali Haji.

Wengine ni Sheikh Hassan Othman Ngwali Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Mahmoud Mussa Wadi Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na viongozi wengine wa Serikali.

Rajab Mkasaba, IkuluZanzibar.